#NilishapatanaNaGod

Nilishapatana na God, na ndo maana sai naenjoy maisha,

Ye ndo Lion of Judah,

Nikiwa na ye sitamani tena kumpata huddah,

Nikisota anapromise kunipa mabunda, ngazi napanda,

Na so soon, sivishwi sanda!

Nilishapatana na God, akabaki na mimi hata waliponiacha,

Coz nilidhani si ni birds of the same feather, kumbe walishaninyonyoa,

Wakaniambia story za early bird na worm, but kabla nifikie hiyo worm si mwewe alishaninyanyua.

Nikawa niko na shati, moja tu, but si then afisa akanishika mashati, na mkono wake uko mfukoni mwangu mwa shati, kumpa chwani masharti.

Movements zao kuumizana ni swift,

Na ni wafast kama maCheetah kudanganya,

Sai mwana mwema, ni normal kumnyoshea mama kidole, sai mwana mwema, ni normal kumkunjia baba ngumi. Sisters na brothers zetu sai wamegeuka kunguni, kazi ni kurukaruka tu kitandani.

But hata binadamu azidi kuwa mnyama, Mungu daima atabaki kuwa wa maana.Na so nilishapatana na God, na ndo maana naenjoy maisha.

Sai nakumbuka, alipatia Elijah chariot, mi naona akinipa chopper,

Israelites walikula manna, mi sai nakula shida but soon nitaishiba, na hicho kiti, one day nitaiown niitwe mwenyekiti, maisha yangu kwao yawe ka bangi, not liking it but using and used to it. Then badae, watavura ka ngano na baking.

Wanasema ati life yangu inasink?

Hawajui anayenibeba alitembea juu ya maji. Wanadhani ju nakula shida nina njaa, nimeshiba juu anayenilisha alifeed five thousand. Na then ati they are sick..of..me, waambie daktari wangu alicure leprosy.

Na kuna time nilikuwa bado mchanga, so machozi yangu yaliponifanya wet, nilibonga matope,

Wakadhani my dream is dead, na kusahau Christ aliraise Jairus daughter,

Wakarankiwa kuwa madictator, na hakuna amewahi fikia Pharaoh,

Then ati my tears have been flowing for years? Waambie Christ alistopisha the flowing blood in a woman. Waliniita kichwa maji, I guess ndo maana sai naflow.

But niwakumbushe tu nilishapatana na God, na ndo maana naenjoy maisha,

Na because of that sai sitalia, coz Jesus already wept, tena sitapatana na uchungu, alichapwa ndo anifie so the pain He already felt.

Sai mi napiga kelele, ye ananena neno moja tu,

Noise pollution nikimake kelele takatifu, waambie waite NEMa wajue kwa God kuna neema,

Wanasema mi ni mWeak, waambieni story ya king David,

Wanasema mi ni mLeast, waambieni story ya Joseph kabla auzwe Egypt.

Wanasema nimejaa dhambi, waambieni story ya Saul kabla awe Paul,

Na ati wao ni maGiant? Kwani hawajaskia story ya Goliath?.

Wengine nao ati ni maSuper Gamblers, wakumbushe story ya wale askari na mavazi ya Yesu.

Na then badae,

Hakikisheni wamejua nilishapatana na God, na ndo maana naenjoy maisha.

#

#FreeVerse254

@s.a.n.d.e.r_o.c.h.y

Author: sander_ochy

I am a journalist, a poet, a spoken word artist, a writer, and performer. Life is all I write about. #Freeverse254

2 thoughts on “#NilishapatanaNaGod”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: