#Orphan?

Kuwa orphan si easy,

Yaani kuwa na simu but call unaeza make ni call for action. Yaani kuachieve success but huna pa kushare, yaani kufail na kukosa wa kukushikilia. Ugonjwa, kila mtu amekuwa doctor love. Kupatwa na njaa,hakuna wa kukulisha,labda wa kukukula.

Kulikuwa na festival, haukuwa na reason ya kucelebrate. Time yenye wazazi shuleni wanapay visits,we ulifeel hata kukosa jina,juu kila mtu amekuwa akikuita “wewe”! Wewe ndo unajua kuwa orphan ni nini. Ila bado ukang’ang’ana.

Wazazi walikuacha ukajaribu kuwapembeleza wasiende ila hawakuchange mind. Ukalia kila day ukitaka their comeback but haungerewind. Ukatamani Mungu angechukuana kwingine kwenye hujui. Sai hukumbuki walienda lini ila unajua ulikuwa bado mchanga, soul yao kwa anga, miili kwa mchanga, ila tena ukakubali waondoke kwanza,ukawaambia ” nendeni naja “.

Ila bado ukang’ang’ana ukamanage kuexcel kwa masomo na juu hukuwa na mzazi wa kukucongratulate ukakumbuka Sunday school ulifunzwa,” God is our heavenly Father “.

Ukasuffer abuse ukiwa mikononi mwa wanawake waselfish,wenye walijali watoto wao zaidi yako, wakawalisha vyakula tamu ila wewe wakakulisha ukoko, wakakutake_in ila badae wakakukick_out. Ukafeel ka uliumbwa kimakosa ama vile uliwanga test tube baby, ukamiss wazazi kwenye awards shuleni, ikabidi umezoea uncertainty na starvation, na badae success yako kwa society ilikuwa kuvunja mwiko.

Juu ya kukosa fees ukadrop out na uliposema urudishwe shuleni unataka kufunzwa, walikuambia adabu ndo hukuwahi funzwa,

Ukasoma na taa haina mafuta taa,moshi yake ikafanya machozi ukafuta, ila bado yote yakapita, na cocurricular, ukacheza futa. Wakajaribu kukugeuza mpira kila mchezaji kukugusa halafu keeper ashindwe kukudaka, ila ukamanage kuwahepa,na mechi ukashinda.

Ukang’ang’ana ukaenda college na juu hukuwa na wazazi, dreams zako ukakosa wa kukupea confidence ati unaeza achieve. Ukafeel kukosa goals, hauna mentor,hauna pesa,haujui maana ya maisha. Ukatamani hata kuwa polisi but corruption, haungewezana. Ukajaribu hata kuoa ila kila mwanamke anachotaka ni pesa.

Ukang’ang’ana na kuenda job interview na ukapita but juu haukuwa na hongo ukaambiwa kuja kesho, kesho ukakuja ukaambiwa kesho, then kesho kesho, na lastly, “tutakupigia”.

Ulipopigiwa uliulizwa ” wi wa ku?” Ukakosa kujibu “mundu wa nyumba” simu ikakatwa.

Simu nyingine ukaulizwa “in ja kanye?” Ukakosa kujibu “jathurwa”, simu ikakatwa.

Ila we ndo yule orphan hakuwahi give up. Juu ulikumbuka una goals, ukaondokea mchezo, ukakumbuka una dreams, ukaondokea usingizi.

Na hata ka walikupiga vita vya kimwili, vya kiroho ulijua na God hawangewezana.Na hata ka ulikosa ugali wa kusonga,bado uling’ang’ana ukasongesha maisha.

Na hata ka ulikosa doh za kurent nyumba, ulijua kwa hii land,God ndo Lord.

#

#FreeVerse254

@s.a.n.d.e.r_o.c.h.y

Photos:_google

Author: sander_ochy

I am a journalist, a poet, a spoken word artist, a writer, and performer. Life is all I write about. #Freeverse254

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: