#UtakapofikaMjini

Mwanangu utakapofika mjini,

wenye utapata huko utawasalimia shikamoo wakujibu fiti, halafu watakuingiza kwa maskani wanaita bedsitter hainanga viti. Sa hiyo ndo watakuwa wanakutake in,ila baada ya muda watakukick out. Utapotea njia na ukiulizia hawatakuambia kwa mdomo, watatumia ishara za mkono.

Mwanangu ukifika mjini,

at times utakuwa low na jinsi ya kuwa high, watakusho ni na mandorm na ati ndo fom. Currency of trade huko ni sex, ju watakuja kwako kuchimba madini ghali, ila afterwards watakulipa na fifty. Watakusho kazi ni nyingi mjini, ila watakayokufunza ni ya uvuvi, wa mavazi!

Kumbuka, huku unakotoka ukiwa nadhifu ulitongozwa, ila mjini kutongozwa itabidi umerombosa. Kumbuka huku usiku ulichapwa ili ulale, ila mjini utafunzwa kuchapa ilale. Ila nakuomba mwanangu chunga, juu huku katii ulicheza,ila huko watakucheza! Huku umezoea kucrush njugu ndani ya kinu, huko utawacrushia then heart yako wataicrush ka njugu, ju watakuwa wamekucheza ka candy crush.

Mwanangu, huku kijijini ulichoacha ni mapenzi, mjini utakachopata ni obscenities, ju huku tulikufunza kuchora vibonzo, but huko utafunzwa kuchora saba. Huku tulikufunza jinsi ya kuwa wife, ila huko utafunzwa jinsi ya kutegemea wi_fi. Kumbuka,umetuaga ukiwa mcool, but ukifika mjini utaonyeshwa styles za kuwa mhot. Huku ulipotumwa dukani ukapoteza pesa, tulikuchapa ili tusije tukakupoteza, ila huko mjini, pesa ndizo zitakupoteza.

Kijijini umezoea kula chakula? Amini usiamini, mjini binadamu hukulana, huku ukiondoka tulikuchinjia kuku, huko utachinjiwa. Kisha utapatana na mapeddi,wakufunze ma_one_night_stendi, then kutojikinga ndo utapata ukedi! Huku kwetu ulikosa fees shuleni ukafadhiliwa na sponsor, ila yule sponsor utapata mjini atakusomesha malimwengu.

Halafu mwanangu,

Huko utapata watu literate wenye standards na wenye hurespect wanawake na kutetea freedom zao,yet rape cases still ziko high. Watu utapata huko ni wenye hubonga strongly kuhusu environment protection, but hawako willing kuchukua farming ka profession, hawawezi fanya jobs za construction. Kazini watakupromise promotion, ila in return watakachotaka ni seduction.

Ila mwanangu naomba, uniahidi utarudi kijijini kama ulivyotuacha.

#FreeVerse254

@s.a.n.d.e.r_o.c.h.y

Author: sander_ochy

I am a journalist, a poet, a spoken word artist, a writer, and performer. Life is all I write about. #Freeverse254

5 thoughts on “#UtakapofikaMjini”

  1. Sometimes I wish that strong messages like we will not just like them and tell the writer what an amaizing piece it is, but we would let the words touch our hearts and we get to spread the message. Anyway, big up brother!!!!

    Liked by 2 people

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: