#Over

Bebi, Darling,
Nakumbuka vile nilikuwa nakuita bebi unajibu “yes darling”,
Kumbukumbu zangu za zile enzi,
Urembo wako ni kweli nilikuwa nimepata,
Ngozi rangi kama ya Lupita,
But dream yangu kukupata ulishaigeuza invalid imepita,
Ka Kemboi nilikimbilia kukupenda, but sai,
Umeniacha narun mad ni wapi naenda?
Vile sai visiting kwangu umepunguza nashuku ile phrase ya no “human is limited”,

Ulikuwanga wangu nikakuita mpeeenzi,
Na kukupenda kisheeenzi,
Ila ni kweli nilikuwa msheeenzi, ukanifanya bumbuazi,
We mkaidi yaani mkia wa mbuzi,
Sifa mbaya hiyo japo sifa ni sifa ulijipandisha ngazi.
Wewe kunitesa na feelings zangu ulidhani we ni queen bee,
Aaaaah aah samahani hukujua mpenzi we ni nzi,

Nilidhani wewe ni kuku kumbe kanga,
Nilitaka uwe mke wangu niwe nakununulia kanga,
Mbona sasa?
Ama ni vile ulidharau kazi yangu ya umakanga,
Najutia hayo sikuyaona, niliona tu shingo yako ya upanga,
Na ndo maana sai you’ve already cut me off your life kama panga.

Mimi nilikula chai na kdf nikijaribu kukaa ngumu,
Ndo wewe nikulishe chipo, pizza na indomie ka mtoto wa sossy
Nilijaribu, vyakula vyako vyote vya kukaanga,
Sikujua busara ndo sikuwahi patanga,
Ama nilikuwa nayo but kidogo ka ya kifaranga,
Bidii yangu hukuiheshimu na salary, yangu kidogo iliyonifanya niizunguke sayari, at times nilihata church service nikaitwa kafiri, ukasahau ya upwa kugaagaa,
Kugaagaa?
Ahaaaaah vile nakuona naona mambo yako yakienda kombo hadi utatafuta mganga.

Kwa ajili yako nilifanya kazi kama punda nikalia,
Kwani uliniona mi pundamilia?
Nikakupeleka shopping Tuskys,
Hukutaka kujua how hard that task is,

At times nilikula githeri,
Mdogomdogo nikifikiria vile nitakulipia mahari,
But hata hukujali kunijulia hali.

At times nikakupatia noti,
Maybe nilidhani ungekuwa mnaughty,
Nikuimbie love songs ka Tokodi,
But madharau yako yakazidi konki,
Nilikufungulia roho yangu but hukukaribia hata kupiga hodi.

Kuna time walinionya marafiki pia na ndugu,
Sikuskia dawa mjinga mimi donda ndugu,
Niliwawakia moto ati vile nakupenda,
Nikasahau ni kweli moto huzaa jivu upesi,
Nilizaa jivu, useless,
Though sai nimeshachanuka, we ni muuzaji gazeti tu,
Mi ni mwandishi niko juu,.

You were once my lover,
But so sad its now over.

Author: sander_ochy

I am a journalist, a poet, a spoken word artist, a writer, and performer. Life is all I write about. #Freeverse254

10 thoughts on “#Over”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: