#Thai

“Na ritwa ria Awa
Na ria Maitu
Na ria Mwene Nyaga
Thai, thathaiya Ngai thai”
Ndizo words zilimark mwisho wa maombi yalotuweka hai
Hiyo time tulikuwanga fiti wallahi
Hiyo time kabla mzungu
Atubadilishie Mungu
Pale pale kwa nyumba ya Mumbi
Kabla mzungu akuje kutukitia kambi
Na kututifulia vumbi
Hakuwa na time ya kubisha
Ndo maana alikuja na bulldozer na kutuvunjia mlango
Alikam na already made up ways za kutudhalilisha
Na kutugeuzia mgongo
Tofauti ni gani?
Alitutoa chini ya mugumo na mlima na kando ya mito
Akatuingiza ndani ya kanisa
Na kutupatia elimu yenye iliondoa wasichana wetu unyagoni
Ona sasa,
Ona vile wao wako free sisi tukiwa slaves
Hawataki hata collabo si tungeunda kitu moja tuiite Black and White
Lakini sa za kwetu hawajawahi tambua
Same case na ile ya black lives
Ona wa kwao wanaitwa daktari
Wa kwetu wanaitwa waganga.
Aaaah natamani “thai thathaiya Ngai thai”.