#DeadAnn

Dedan, amepatana na Ann
Alikuwa mshukiwa wa kufuata ile njia ya gun
Naye Ann alikuwa wa ile njia ya kuearn
Na ile njia ya kutumia fun
Kwa ile business yenye sponsors ndo wanarun
Juu ya kuwa wasted akanicknamiwa ‘dead Ann’

So Dead Ann alifall in love na Dedan lakini kama ingekuwa long lasting hakuwa na guarantee
Akaconfirm from neighbors wakisema so soon atatii
Haya
Ilianza na Ann kumsho ‘acha ufala’
Naye akamjibu jifanye tu mjanja
Ann akamwambia ‘uko na umama’ naye akamsho ‘speak back to me if you are man enough’
Dedan akauliza ‘are you mad?’ Naye akasema ‘you are crazy’
Akasema ‘let me clean up the kitchen’ akaambiwa ‘clean yourself first’
Akaongezea ‘behave like a woman’
Naye akamsho ‘man up my friend’

Okay,
Ni kweli Ann alikuwa amezoea kupigwa kuni
Akakam kwa Dedan akampiga na kuni
Ati juu ya maringo choo za ushago hakuni
Sai vile anaangaliwa, macho wide ka za mbuni

Ni kweli Dedan alikuwa on drugs
Mdomo green
Macho red
Mapua grey
At this point angegeuza yeyote prey
Alibonga sheng’ sana Kiswahili kifukuzwe akiSanif
Akaanza kumvuta Ann kando, juu chini ni ka alikuwa anamfrisk
Akiteta vile alikuwa anaangaliwa Ann alifeel at risk

Hungedhani ndo wale mbeleni walikuwa wanalay their bodies together kwa bed
Sai ni laying his hands on her
Vita alimpiga hakujali the treasures beneath her blouse

Na ni kweli chenye Ann aliona ama ni ndoto tu?
Alimuona amelala kifudifudi na chini yake kuna dem alikuwa amelala chali
Anajiconvince Ni God’s plan sio ajali

Na ni ukweli alivyosikia Dedan ati uko kwa streets Ann huongea uongo na wale maLiar?
Ni nini hicho Dedan anamwaga nje na Ann ako sure sio libation?
Ni mzinga gani hiyo Dedan anabuy na Ann ako sure hafugi nyuki?
Marafiki wa Dedan walikuwa wabaya, kwa Ann walikuwa ngano na ye alifeel kuwa lupita, alitaka kuWakanda

Sai anakumbuka vile mbeleni walipromisiana kuishi in one peace
But there was no piece of peace that they ever used
Haingewahi isha wakiwa at ease
The last words alisema ilikuwa please
Mbeleni walikuwa wanakiss
Sai ni kudiss

Ni at this point ndo Ann alimuunderestimate
Right from where he lived to his manhood
Sai anafeel kumuacha but angefanyaje huo uamuzi na amelewa si ingekuwa impaired judgement?

Dedan alimpiga Ann
Alimpiga na kila kifaa
Feeling ka ya Yesu kutembea juu ya maji but sai ye alikuwa anawalk on her own blood mumewe akiwa maji
Akapata guts za kumsho Ann hakuwa na haja na yeye tena
“So you only needed me for sex?”
‘huh, you are just like my ex

So ikawa hivo
Ile ndoo Dedan alimpiga Ann nayo kwa kichwa ilimfanya apige ndoo teke

Sai anashangaa kama atawahi sema “yes I can”
Ama ajipate amesema okay it’s done
Juu ni kwa ile njia tough ndo amelearn
Joto amepata ungedhani ako kwa frying pan
Ana words confusing hadi utadhani ni pro wa kupun
Alikuwa ready for transformation but was still on the run.

Author: sander_ochy

I am a journalist, a poet, a spoken word artist, a writer, and performer. Life is all I write about. #Freeverse254

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: