Utamu wetu usiwahi kuwa chungu
Tayari nishauonja
Macho yangu hujaa ukungu
Ninapokuona kwenye toja
Nishapima akili yangu
Ulimi wangu wakutaja
Usiniambie wewe ni dadangu
Nishawahi kuona kwenye paja.
Tazama naandika huu utenzi
Tabia ninayoionea fahari
Kukuonyesha ninavyokuenzi
Siku moja nitakulipia mahari
Ninayoandika ni jinsi ninavyo mapenzi
Yalonilewesha chakari
Yamekuwepo kutoka enzi
Usiniambie kwaheri.
Kesho jitayarishe
Nakukujia
Twende nikulishe
Bajia
Nikukumbatie hata tukeshe
Kando ya njia
Fumba fumbua nikuchekeshe
Hayo daima tarajia.
Wow that’s👍
LikeLiked by 1 person
Thanks so much 🙏
LikeLike