#Ghetto

Ile ni grao ya ya khati
Na ile ni ya futa, na ile ni ya reso
Zile bushes ni grao ya birikicho
Mimi ni pro wa kugeuza matchboxes into playing cards
Mimi ndiye nilikuwa referee wa bano hapa kwa hii ghetto
Kwa mdomo nachew collar ya shati nikijitayarisha kutoa uamuzi wa ni timu gani kali hapa
Mimi ndiye kusema, lakini si ile time mama ako around
So leo nimeamkia news za kale kadem kangu Sheila ati malnutrition imekaua, kwa nini?
Wallahi?
Siamini.
Anyway, cases ka hizo tumezoea hapa.
Mama, wamekuwa zaidi ya watano hii wiki babangu ni mgani?
Ama hiyo story nikanyagie yaani
Haidhuru
Nafungua mlango kutoka nje, aah nyumba yetu haikuwa na mlango na tulifeel so secure tusibishane
Hakukuwa na dirisha, ata ungefeel kujoin spotPesa ndo uWinDoh
Hapo nje naona cuzo yake Sheila kwa mkono ako na manati
Sijui nini ama nani anataka kuaim but ni ka ako out of stones
Mkono ya left ndo imeshikilia sengenge ni kama he’s the boy on the fence
Miguu yake tupu ni aje angeBear hiyo pain?
Machozi inampa blurry vision ni aje angeoversee his future?
Rubish imetapakaa kila pahali anashangaa mbona kuishi hapa wazazi waliTaka
Ni nini hicho kingemzuia kuwa pedi na alitaka kuwa juu ya wengine?
Sai hana hadi zile sleepers za bata, angeafford aje kuku?
Anawaza sana ungedhani anaload airtime vile kichwa alikuwa anascratch
Hii ni ghetto anyway.
Niko hapa
Hapa ghetto
Sielewi mbona joto la kifamilia la kisiasa linazidi
Niaje nahisi joto sana na hip-hop mi ni fan?
Politician wetu hajawahi tembea juu maji ka yesu but niaje tunamPraise?
Ni lini last nilikula? sikumbuki
Hii ni ghetto
Yenye wanadai hawatanibetray na already washanikiss
Hawawezi nideny but already jogoo ashawika
Ghetto naumia, nitafunguaje roho na wameninyima spanner?
Kusota imenihit design mi hubonga na poverty like we’ve ever met before
Sijapata job bado but ni juu kila time nikitafuta mi husahau kutoa hongo
Sai hapa nina nia but sa wa kunionyesha njia ndo sina
Hapa, penye mwizi wa kuku huhukumiwa kifo na mwizi wa uhai anahukumiwa kuchunwa sikio
Penye madem night hours ni chuma moto
Utadhani wao ni Zakayo venye wako juu ya miti
Machali nao night hours kwa belt ni chuma baridi
Hii ni ghetto
Baridi, njaa, joto, wizi, abortion, kipindupindu, suicide na risasi ndo life ya hapa ghetto.
Thank God tulisurvive.

Author: sander_ochy

I am a journalist, a poet, a spoken word artist, a writer, and performer. Life is all I write about. #Freeverse254

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: