#NewWay

Juzijuzi tu amekuwa toddler
Damu mbichi so innocent
Born akiwa star
Hakuna ambaye angedhania angekuwa stu-bborn
Mamake alikuwa ndo Nerea na aliwitness akikam na sahani na akahope life yake itajawa na amani
Hakuwa na baba wa kumlipia further studies
Na mamake alifake it, so hakutambua mother nature

So
Shiko alipofika hiyo age aliamua kwenda Nairobi kutafuta furaha
I wish angejua ata angeenda Nakuru angepata Afraha
Akawa yule dem wa class
Kukuangalia tu within two minutes ashakusoma
Ungekam kwake bila outfit
Aki ya Mungu angekutoa out hungefit
Social media alikuwa celeb na followers wengi japo maadili hakufuata
Pale twitter, alishindwa kuwahandle
Hakuwahi fika Israel but alijiita mgaza.

Alipenda kuupdate playstore, ndo ilimfanya akuwe h-appy
Ye ni yule mdem atachagua food mchuzi
Ju ye huwanga choosy
Highschool hakufanya agriculture but ye ni expert wa weed na kupanda miti
Siku zake ziuwanga type mbili: kuna zile safe na zile unsafe.

Boy wake alikuwa wa kustone- Stone-Boy
Ama ukipenda wa kuburn-BurnaBoy
Boy mwenye alifanya na yeye mapenzi kinyume cha mapenzi
Boy msimple aliyeitwa Stivo but sa shida ni ati alitumia mihadarati
Boy mwenye kila dem, angemSmackDown Raw
Boy mwenye kwake alifaa kuwa therapist
But instead akaturn out kuwa the-rapist.

Sooo
Shiko amesahau kushika kijiko sai anashika kiko akivunja mwiko
Badala ya kuvuta pumzi sai ye huvuta bangi
Yule mdem mwenye alikuwa student mbright vidifferent
Sai amepata D akitafuta rent
Ofcourse hakufunzwa na njia ya ukora
But sai kila kona akipiga polisi wanamsorora.

Kila time ye hujipata kwa ngori
Hakumbuki the last time alisema sorry
Akianza alikuwanga dreamchaser
Sai ye ni yule mdem wa makali bila chaser
Vile sai alikuwa na maboy wengi
Ata ungeshangaa kwani ana roho ngapi
Na akili light ka mtungi empty
Kweli furaha angeitoa wapi
Na last month anakumbuka hakuflow
Anashangaa kwani amebeba kijusi!
Na vile ata hajawahi pimwa sai anafeel ka ana maumivu.
Alivaanga wristwatch but kila day aliwanga out of time ni maquickie
Hakuwa referee wala hakuwa na whistle but alikuwa ule wa kublow
Hungewahi muona na bike but sai alikuwa pro wa kuride.

Hapo mbeleni ungempata amefunga leso
Mbele ya wazee akipata lessons
Sai ye hufunga leso mbele ya maboy akitaka ile mchezo.

Na for so long alitrainiwa kukaa akiwa virgin
Hakumbuki mafunzo ya kupenda hii maji
Innovation ndo aweze kujitafutia ganji
Sai ako idle beshte yake ni cannabis
Hajui hata ka ana kipaji
Kila kitu akijaribu ni I can’t do this
Her highness is so fake ka ya watu wa vela
So fake, ka nyuma ya Vera.

Kitambo ungemuattack angejipa defense
Sai hadi hajui ako wapi she’s the girl on the fence
Alisare story ya kukaa kwa kambi
Akitafuta wazee wenye vitambi
Sai anaishi kwa ile state ya hali sio hali
Although chenye kilikuwa kwa mind yake ni kupata mali
But ikamwacha kwa state ya kuvua suruali
Kwa moyo wake ashaanza kupata scar
Hadi anajiskia kuwa fan ya wakadinali.

Ashaanza kuona familia ikitumiwa rambirambi
Anashangaa nani atamuokoa
Anafeel amebeba nyingi dhambi
Angekuwa na uwezo angezikohoa
Kila kitu anaona hakimbambi
Anatamani ile siku moyo utapoa.

Amekuwa akidanganywa na texts za songs of Solomon
Kumbe ndani yake ni vitisho vya Revelations
Sai chenye anafanya ni lamentations
Ameshindwa kufumbua proverbs za hii life na so anafeel ako tirePsalm.

Depression imempeleka hosi
Na ni kweli hiyo Graph
Ilionyesha afya yake ilidrop na speed Khali
Akafeel ujanja wake umeisha
Ujanja wake wa sungura kuchanganya hao makaka, wenye alikuwa akicheque their cash
Ujanja wa nyani, leo amefika jangwani
Hana usaidizi kashikwa na nyama mdomoni
Anafikiria kurudi nyumbani kupreach changing ways
Kumbe hakuna cha charity begins at home
Anakumbuka ye ni prophet na huko ni hometown
Sai sa kila siku ni suicidal thoughts
Anaandika suicide note anaWrite to die.

Anafeel ka ako undersea
Vitu ameona kwa hii dunia wallahi hawezi unsee
Anafeel so tiny, masterd seed
Anashangaa kama atawahi kuwa a big tree
Sai ye ni mifugo bila pasture
Chenye anapitia sai, torture.

Anakumbuka vile beshte zake closer walikuwa wanampull
Sai hawako naye tena nine months later wanampush
Walikuwa magoalkeeper na yeye mpira
At first walimhug tight, then wakampiga teke
Tunnel yake huko mwisho haikuwa na light
Imeziba ni wapi atachukulia hiyo flight
Amepatana na noma mob hadi anashangaa kama atawahi kuwa wife
Vile tu ameteswa na pain kwa hii life
The only option ako nayo ni ile pain ya knife.

Soo
Shiko, aligo through this hadi ile time aliskia kuhusu Christ
Hakujua Jesus ni beshte alimpenda that much.

Aliskia kuhusu zake miujiza
Kabla amjuwe Christ alikuwa already ashamsearch.
Before azaliwe God alikuwa ashamjua
Before agive up God already alikuwa na plan
Plan ya kumuokoa, kutokana na madawa na beer
Plan ya kumsahaulisha zile mara mob ameumia
Plan ya kumpatia ile happiness amekuwa akitaka
Plan ya kumuinua, kutoka kwa jaa la taka
Plani,
God alikuwa nayo ya kumpa longlasting peace na life everlasting

Sai anafeel ni wa Jesus kama Kabi, na ameamua life pamoja na God, ndo itakuwa her #NewWay.

Author: sander_ochy

I am a journalist, a poet, a spoken word artist, a writer, and performer. Life is all I write about. #Freeverse254

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: