#Mui

Najua umejawa na kinyongo,
Unatamani uniuwe,
Usichojuwa ni sina moyo,
Badala yake nina jiwe,
Kiporo ni wako uchoyo,
Ulokauka kuliko tumbawe.

Endelea kunichimba,
Nipige pia na vijembe,
Navyoona unayo mimba,
Kitakachozaliwa ni uzembe,
Waugua moyo wenye magamba,
Katu siumezei tembe,
Ngozi yako kama ya mamba,
Haikatiki hata kwa nyembe.
.
Nishakuzoea na wako ubatili,
Haujamjua mungu we bado kafiri,
Ila unamjua ibilisi ashakufunza ukatili,
Alishakuchanganya na akili,
Na kukupa fulani umahiri,
Umahiri wa kutokubali,..
Kuwa kuna njia halali,
Za binadamu kujipatia mali.

Ulijaribu kujisawishi kwa kuvunja watu mbavu,
Na sasa unajaribu samaki kumkunja hali yake kavu,
Paukwa, pakawa pako pakavu,
Umenuna, wenzako wote ushawavurishia shavu,
Ulidhani utawaumiza kumbe wewe ndo ungebaki na kovu.

Unachozungumzia ni shibe na jirani hajakula,
Usingizi na siku mbili jirani hajalala,
Sahau ata kulala pa kulala ndo balaa,
Katu hadhani kama atawahi ondokewa na ufukara,
Yeye na familia ni hisia za kuku kuchakura,
Ashachoshwa na mambo mengi hasa misimu ya kura,
Madeni anayo hadi Tala,
Kila kukicha humpigisha sala.

Tabia unazofanya hazifai,
Unaishi kama usodhamini uhai,
Kutembea na unakoenda hujui,
Iwe ni masimulizi au umbea hautambui,
Ila nachokuombea ni rai,
Jaribu kuwa mwema katu usiwe mui.

Author: sander_ochy

I am a journalist, a poet, a spoken word artist, a writer, and performer. Life is all I write about. #Freeverse254

6 thoughts on “#Mui”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: