#BinadamuMimi

Mimi ni binadamu,
Yaani mwana yaani mtoto wa Adamu,
Kila kukicha naamka kwa hamu,
Hamu ya kupatia maisha utamu,
Japo huo utamu naskia huja kwa zamu,
Wengi washaupata wakapoteza fahamu,
Na kuishi kwenye bahari ya raha na karamu,
Ila wanaojua hali yangu,
Huniambia Mungu ashaiandika chini kwa kalamu.
.
Nina marafiki, familia na majirani,
Wengi nawajua wengine hatujuani,
Ila wote wapo duniani,
Na dunia hutegemea matumaini,
Ni kweli matumaini ni mazuri maishani,
Ila nachotaka niambieni,
Nitategemeaje jua na nipo masikani?
Ni kweli nishavunjika moyoni,
Ninayoyatarajia hatupatani.
.
Mzee wangu aliniambia nyumbani,
“usiwahi hisi kuvunjika moyoni,
Hakuna ambacho hakiwezekani,
Magumu huwa hayakuji kudumu,
Na una kila sababu ya kushukuru,
Jipe moyo hata kama unachoma mahindi ngara,
Usikate tamaa hata kwenye siku zako za kuparara,
Kuna nyota hung’aa zaidi ya zingine,
Na ziking’aa hazidharau zingine,
Kuna wengi wenye malengo,
Yaliyosimamishwa kama yaliyogonga mjengo,
Chunga baraka usiyageuzie mgongo, Usiwahi fikiria kwa hii dunia kuacha pengo.

Author: sander_ochy

I am a journalist, a poet, a spoken word artist, a writer, and performer. Life is all I write about. #Freeverse254

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: