#SiSasa

Binadamu tumekuwa wanyama, na si victor,
Mali yote tunapata ni kwa njia ya ngeta,
Wanaume wanapractice cannibalism,
Badala ya kuungana kusupport feminism.
Kwa sababu ya success kukam polepole ka kinyonga,
Msee anaamua tu kujinyonga.
Maboy under twenty wanaface detention,
Madem under twenty already wanabenefit from pension.
After boy amegeuka wa kukabana koo,
Girlfriend yake anaamua kutupa mtoto kwa choo.
Anakumbuka vile alikuwa akishikanishwa na ukuta,
Na kulia vile ashageuka mwanamke faster.
Chenye kimekuwa topic sai ni masculinity,
Na watu huko nje wanaloose humanity.
Madem sai badala ya kutekwa,
Sai wanatekwa, nyara.
Masomo bila malipo,
I guess ndo maana wamekuwa kama popo,
Nusu mnyama, nusu ndege ndo maana anaweza au kukosa kubeba lawama,
Mtoto msichana, anaogopa kusomewa baada ya kusoma.
Na kuna mtoto aling’olewa pahali,
Hakupata chance ya kuishi na pengine angekuwa daktari.
Hakupata chance ya kuoa au kuolewa,
Angeishi labda ata ndo angekuwa miss Katiwa.
Gava imejaribu kuingilia kati,
But majibu ya maswali tunauliza wanadai hawapati.
Chenye najiuliza, ni kwa nini bado kuna drug trafficking? Angekuwa hai ningemuuliza Saitoti.
Kwa nini bado kuna violence time ya elections? Angekuwa hai ningemuuliza Musando.
Walipata power wakajiona wamighty,
Na kusahau kuna day itakam wageuke maiti.
Sai wanafloss na doh mob,
Na kusahau kuna time wanaweza jipata wakitumia mop.
Wana mabunda, I guess ndo maana mtaani tunawaita mabuda.
LAKINI ninachoamini ni kuwa siku ya kusmile inakam though si sasa.
Ju sai nina cousin anaitwa Job na hana kazi.
Beshte yangu anaitwa Hope na alishapoteza matumaini after kugive birth to Precious mwenye sai maisha hayana dhamani kwake, na best friend yake ni Angel though tabia zake anashuku hazitamfikisha heaven.
Time ya kusmile inakam though si sai,
Ju sai bado hadhi tunashushwa,
Bado malegend wanaangushwa,
Bado wasichana wetu hawajaacha kuliwa,
Bado wasichana wetu hawajaacha kuuliwa,
Hizi tabia tunaziona zimekomaa,
But still kuziongelea sitakoma.

Author: sander_ochy

I am a journalist, a poet, a spoken word artist, a writer, and performer. Life is all I write about. #Freeverse254

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: