#Marked

Hey Cancer ,
Ni kwa ajili yako ndo nimeandika hii stanza,
Naona umeanza uchokozi sasa,
Si unakumbuka penye alikuwa ameketi we ndo ulimpata?
Ukamfanya aanze kutapatapa,
Kila hospitali akitafuta tiba,
Kumbe ulikuwa unajua already ata afanye nini ulikuwa ushamganda?
Ukamwacha, alipotuacha, Ukaenda kwingine, kuwindana harakaharaka.
Haukumuuliza ata alitoka wapi,
Na ulijua vizuri alikuwa zawadi toka mbinguni,.
Cancer kwani,
Kwani hufikirii ameacha nyuma kina nani?
Wazee, wachanga, wengine humuita Nunny,
Kwani, majonzi aloacha nyuma huoni,?
Safari yake ulikatizia nusu barabarani,
Cancer tafadhi ondosha kisirani,
Tushakujua we ndo aka saratani.
For sure aliowaacha life imewafanya tough,
Kuwa tough kumewakeep alive.
Na kulikuwa na mtoto mdogo aliyembeba,
Sai hana mzazi kwa palm yako ushambeba.
Alimtunza sana akiwa mchanga,
Unadhani atafanyaje hivyo akiwa kwa mchanga?
Ni sawa nakubali huyo ulimchukua uzeeni,
Lakini yule alikufanyia nini na alikuwa under eighteen?
Cancer mi nikikuskia mi hufeel kutapika,
Ushachukuana huko, Kule, wakujia nini huku kwani hujatosheka?
Kwenye ulianzia machozi bado yanatiririka,
Ju we kila pahali unapitia huacha wakisononeka!
Tulikugundua mapema na ndo maana udongo tukauwahi,
Lakini we ni monster ulituzidi nguvu wallahi!
Kabla umpate tulikuwa tunajibamba weekend,
Ona sasa ulivyomfanya weak in the end,
Alifuga ng’ombe aliopenda kupeleka kwa slaughter house,
Ona sasa umemslaughter in her own house.
Na alikuwa tu mstrong, ka cyborg,
Half human, half amazing.
Ila sasa ashaenda hayupo machoni,
But daima atabaki kwa akili na moyoni.
Na nakumbuka kabla aondoke ulivyomweza,
Tukamtia nguvu, na kumwita fighter,
Tukamwita strong woman,
Tukamwita warrior,
Ila yeye alijua hangekuwa warrior over cancer,
And she couldn’t just stop thinking of death japo hakusema.
Ila juu ya waliozungumza sana kwa hali yake alisema.
Na akasema:
Once my hair is gone,
Once I can no longer taste my food the drinks leave alone,
Once I have passed out while shopping for bread,
Once all my ex lovers have visited me for memories we best had,
I have become a patient,
The old days are gone,
Every corner of my room is made of medicine,
I am marked by cancer, and I can’t quite remember what the markers are that mark us, us with cancer as who we are when we are not being marked by something else.
Akalia machozi Kisha akaongeza:
I won’t give up,
I won’t give up untill I give up.

Author: sander_ochy

I am a journalist, a poet, a spoken word artist, a writer, and performer. Life is all I write about. #Freeverse254

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: