#HerHopeIsBack

Alifanya mengi mabaya,akasahau mengi mazuri,

Akasahau giza haiwezi ondoa giza,mwangaza huondoa giza,

Ndo maana aliishi na moyo wa kulipiza kisasi,akasahau kuna tofauti ya kupiga story,na kupiga udaku,na ndo maana aliishi kuzurura akisambaza duru za kuaminika.

Vile hii life iliwanga imempararia,alifeel kuihama hii dunia,

Yaani kwa nini,kwa nini yaani,

Cheki,

Dadake mdogo aliwanga ashaanza kukatiwa akiwa 14 na wazee wenye waliwanga ndani ya makoti,na hata hawakupelekwa kwa koti ju badae wangetoa ile kodi,ndogo,ya mlango wa nyuma usiokuwa na kochi,badae akakata roho akijaribu kuavya mimba kwa ploti,..

Dream yake ya kufanya Education P1, ilipotea vile mamake alishamfunzanga kutumia p2,.. Yeye na wenzake wakarefusha foleni kwa vct akaingilia prostitution kupatana na mental abuse,violence, torture na then police station kujaza p3,. Pesa kwake iliwanga sabuni ya roho,Ila tena ilimchafulia maadili..

Okay,

Si hayo tu yalimfanya aloose hope, kaka yake mkubwa aliwanga ashafungwa jela miaka mbili kwa kumtia mtoto wa shule mimba, alikuwa ashatumia drugs hadi akili imemruka, Nyanyake sai anaugua kwa kuendewa sivyo na nguvu za mganga, kila mtu anamlia but wengi wao ni machozi ya mamba, sai Anajaribu kujaza kibaba but anashangaa ataijazaje bila hiyo haba,

Babu yake alishakula taabu, akaaga na kumwacha bila mtu wa kumfunza adabu, akajizoesha kutembea juu ya miiba bila viatu,akadungwa,akavura,after nine months akapona,.

Akaloose hope, akawa anastay long kwa dancefloor so that she could sweat the stress out,

Hakuwa anapenda samaki,but hii life iliwanga imemhook kwa line ya the wicked,

Akageuka mbuzi,kuendaga casino kuchew card,ndo akashinda lottery, akapeleka 10% kwa church akawa amepatia God fungu la gambling, fungu la ngumi, coz aliwanga amesahau lile la kumi halipatikani kwa njia za mkato,

Alikuwa amechoka na haya maisha, ju ye sai ndo aliwanga mlevi wa jiji,na Yale yenye yaliwanga yakimhappenia kwa life yake sai,alijua wahenga walikuwanga washayaona kwa macho ya kitambo,

Alikuwa akipiga kelele kwa ulevi but then alijua God ni msoh, angemfanya aache kupiga iyo kelele chafu, aende bafu,aoge mwili na roho ndo aanze kupiga kelele takatifu,

Alikuwa amechoka na haya maisha, ju akiangalia kushoto kulia anaona vijana ndo sai wanatumia mikongojo, pizza na burger zimereplace ugali na madondo,.maboyz, sai wamekuwa wakali kushinda wembe, na ndo maana wanashindana, kukatiana.

Anakumbuka haya maisha ndo karibu yafanye Job aache kuitwa the patient, shetani karibu amfanye aloose Patience,

Anakumbuka haya maisha yamejaa lust na greed na ndo yalifanya yesu auzwe, yakahangaisha Israelites hadi kutamani kurudi Egypt, yakafanya Elijah aogope Jezebel,.

Sai anaskia wakisema ati maisha ni mafupi, yolo, ati jibambe Leo unaweza ukafa tomorrow, ati bora usizue migogoro,

but haelewi mbona siku zake ziuwanga ndefu, anaona wenzake wakiflap flap flap, na anawaona wakifly na ye sai ndo anajifunza kucrawl,

Ashaanza kujua she’s not perfect, but still anajua God alimcreate in His own perfect, image akampa mwili ya kuimonitor awe prefect ,,sai anajua she’s full of mistakes but pia anajua God akimcreate haikuwanga mistake, sai still anakaa still,akiwa mgumu kama steel, ju anajua still, waters run deep,.

This time anajipa hope,

Anajipa hope ju ashajua ati watu wote wako kwa mashua moja, dunia,maisha ndo bahari, troubles ndo mawimbi, Ashajua wanaomkataa Christ, sai wanadrawn, na ye anafeel kufloat ju ana lifejacket, Christ,

This time kwake nyangumi na papa zikimvamia anajua God ndo baba, Ata zikimmeza, anajua bado atafika, Nineveh bila njeve, ka Jonah, _anafeel atapona,_strength ka ya Samson anafeel atashona, _busara ka ya Solomon anafeel atasoma,

Church sai kwake ndo center of worship, Jerusalem,_anafeel kuishi in the home of kings,Kenyan Bethlehem,.

Sai anafeel hayuko chini ya jua,ako chini ya mwavuli na mwamba, Christ anambambaaaa mbaya,

This time badala ya kuhung out na agemates wanadream insanity wakismoke weed,

ye hukesha church akismoke incense and in sense.

©s.a.n.d.e.r_ochy

#FreeVerse

Author: sander_ochy

I am a journalist, a poet, a spoken word artist, a writer, and performer. Life is all I write about. #Freeverse254

4 thoughts on “#HerHopeIsBack”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: