#DuniaHii…

Na dunia ni kama imefikia kikomo, coz sai hewa imepollutiwa, maji yamecontaminatiwa,, Wanyama wanaendelea kuwa extinct, economy imecollapse, masomo yamekuwa mafupi na polisi corrupt Intelligence imewekwa chini ya carpet na ignorance imekuwa rewarded Sai watu wanakaa depressed na hasira,hatuwezi ishi kila mtu na mwenzake,hatuwezi ishi na sisi wenyewe, kila mtu ni mgonjwa. Na dunia ni ka imefikia kikomo coz sai kila msee anataka zile 15min of fame,ndo unaona kwa front-page ya star, msando, Pendo, another fallen star, Watu sai wanataka fame kuliko kuwa na meaning na purpose, kwa sababu kile chenye kiko more popular kiko more important kuliko chenye kiko right, ratings zimekuwa more important than truth. Sai ndo serikali inajenga shule moja, magereza matatu,. Viwanda vitatu vya kugenetically modify organisms, na hakuna hospitali ya kutibu cancer,. Serikali inajenga dams za maji ya agriculture, na politicians washatunyakulia mashamba. Sai mapresident wanatudanganya, politicians wanatutrick, political temperatures wanaziheighten, hakuna msee ako willing kuwa enlightened,coz life ya kila mtu iko threatened, na hawa mavoucher hakuna mtu wa kuwafrighten kwa sababu courage yetu na power walishazigeuza their begotten, Kenya imekuwa a kingdom forgotten. Sai wametubrainwash,hakuna tunayemtrust,wametufunza kutotambua brothers na sisters zetu. Wametufunza kuonyeshana hasira,chuki na cruelty. Sisi wenyewe hatuongeleshani tukipatana, na tukiongeleshana tunaongea juu ya vitu meaningless. Ukabila bado ni issue, and so is religion, ati God wako haexist,wangu ndo anaexist na ukidisagree na Mimi ndo tunakosana. Na dunia ni ka imefikia kikomo, coz sai ngoma zenye tunasikiza 90% ni about sex ,watoto sai wameacha kucheza tag of war,wanacheza twerk videos.wanaspend more than 5hrs kwa TV na kinachoonyeshwa huko ni jinsi ya kuleta violence. Technology imetupatia kila kitu tunachohitaji na at the same time imetuibia kila kitu tunachohitaji. Pride imekuwa at all times high,humility at all times low.kila mtu anajua kila kitu,kila mtu anaenda kila mahali,akiignore mtu,akiblame mtu. A lot of human doings,mental abuse,violence na torture,. Manipulation, rape, hunger na horror. Pesa nayo is still the root of all evil,

Issue ya kutenda wema nenda zako hakupo tena, wema unafanyika pale penye margin ya profit. Na dunia ni ka imefikia kikomo, coz sai picha za wale misfortuned zinaenda viral,. Tunazishare na kucomment,kisha tunacheka online. Marole model wa sai kitambo ndo waliwanga bad examples. Sai ndo mwalimu anakatia student kwa class, sponsorship imekuwa na more than one meaning. Izi ndo days zenye shisha zimeshikana na seduction, fornication, tabia hazifanyiwi close supervision, then after poverty, abortion,.

Izi ndo days zenye kutoa mimba tena si motion na after hiyo abortion stretchmarks zinatolewa tumboni na body lotion. Na si ka ingekuwa kitambo aborters wangeexpelliwa na kufanywa homeless and forever worthless.? Na dunia ni ka imefikia kikomo, coz sai love imewacha kuwa blind. Love inaona. Inaona senti kwa benki na inaona haggah na beauty, inaona status na riches na ikishaona hizo inaingiza na jealousy. Hizi ndo days zenye tunaishi na hatred na hata sokoni sai ukifika hakuna barter trade. Virginity imewacha kuwa sacred na life of man imewacha kuwa priceless. Tumewacha kuabudu mungu,tunaabudu dini Wanaume hawaeleweki Wanawake wamekuwa wasagaji .makampuni yanainvest mamilioni kuhire specialists kufanya wasichana wadogo wafeel kuhitaji makeup kuwa warembo,na kuwafanya wawe na self esteem ndogo,coz they will never be pretty enough. So dunia ju inafikia kikomo, tufanye? Tunaweza pendana, real love, true love, boundless love. Tukipendana ,tutameet hasira na sympathy, tutameet chuki na compassion. Tutameet cruelty na kindness .

©s.a.n.d.e.r_ochy

#FreeVerse

Author: sander_ochy

I am a journalist, a poet, a spoken word artist, a writer, and performer. Life is all I write about. #Freeverse254

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: